Sifa Za Kujiunga Na Chuo Cha Uhasibu Tia, Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) kinatoa programu mbalimbali kwa wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu. Ili kuhakikisha mchakato wa maombi unakwenda vizuri, ni muhimu kuelewa masharti mahususi ya kujiunga kwa programu unayotaka.
Hapa chini kuna muhtasari wa sifa hizo:
A. Sifa Za Kujiunga Na Kozi Za Cheti Cha Awali (NTA Level 4)
Mwombaji awe amefaulu angalau masomo 3 kwa kiwango cha alama āDā au zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne
Au awe na cheti cha mafunzo ya ufundi daraja la pili (NVA 2) kutoka chuo cha VETA, mwenye ufaulu wa masomo angalau mawili katika kidato cha nne
B. Sifa Za Kujiunga Na Stashahada (Diploma)
Mwombaji awe na cheti cha mtihani wa elimu ya sekondari (CSEE) chenye angalau ufaulu wa crediti tatu na kufaulu Hisabati na Kiingereza
Au awe na mitihani ya Taifa ya Biashara NABE stage I & II na angalau ufaulu wa masomo manne na cheti cha elimu ya sekondari
Au awe na Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) yenye angalau ufaulu wa principal katika somo moja na subsidiary katika masomo yanayohusika, lakini ni lazima awe na ufaulu angalau wa Kiingereza na Hisabati katika elimu ya sekondari
C. Sifa Za Kujiunga Na Shahada (Bachelor Degree)
Mwombaji awe na Advanced Certificate of Secondary Education (ACSEE) graduate na ufaulu wa angalau principal mbili
Awe na jumla ya pointi 4.0 katika masomo mawili yanayohusika katika mitihani ya ACSEE
Kuna masharti mengine mahususi kwa baadhi ya programu za shahada ambazo ni lazima yazingatiwe. Ni muhimu kuchunguza programu unayotaka kujiunga nayo kuhakikisha unatimiza vigezo vyote vinavyohitajika https://www.tia.ac.tz/.
Sifa zaidi:
Tuachie Maoni Yako